Jinsi ya Kustahili Kupokea Msaada wa FEMA Wakati wa Majanga: Matakwa ya Uraia na Uhamiaji

FEMA na serikali ya jimbo, eneo au makabila inaweza kutoa msaada wa majanga wa moja kwa moja na wa kifedha kwa raia wa Marekani, wananchi wa Marekani na wageni wanaostahili.

Msaada wakati wa janga unaweza kutia ndani kupata pesa kwa ajili ya kulipia kodi kwa muda mfupi, kurekebishiwa nyumba, mali ya kibinafsi iliyopotea, matibabu, gharama za mazishi, na mahitaji au gharama nyingine kubwa zinazohusiana na janga lililotokea ambazo hazishughulikiwi na bima au njia nyingine.

Waathiriwa wa janga, haijalishi hali yao ya uraia na uhamiaji, wanaweza kupokea huduma zifuatazo ikiwa zinapatikana: rasilimali za kutegemeza uhai kama vile makazi, chakula na maji, ushauri wa jinsi ya kukabiliana na janga, kushughulikia hali za majanga, kupokea lishe ya ziada na huduma za kisheria.

Ufafanuzi

Raia wa Marekani

Mtu yeyote aliyezaliwa Marekani; mtu yeyote aliyezaliwa nje ya Marekani ambaye angalau mzazi wake mmoja ni Mmarekani; au raia wa asili.

Wananchi wa Marekani

Mtu aliyezaliwa katika milki ya nje ya Marekani (yaani, Samoa ya Amerika au Kisiwa cha Swain) siku au baada ya tarehe ambayo Marekani ilipata milki hiyo, au mtu ambaye wazazi wake ni wananchi wa Marekani. Raia wote wa Marekani ni wananchi wa Marekani, lakini sio kila mwananchi wa Marekani ni raia wa Marekani.

Mgeni anayestahili inajumuisha

  • Wakazi halali wa Kudumu (wanaomiliki “Kadi ya Kijani”)
  • Wageni waliopewa hifadhi
  • Wakimbizi
  • Wageni ambao hadhi ya kufukuzwa imezuiliwa kwa angalau mwaka mmoja
  • Wageni walioachiliwa nchini Marekani kwa angalau mwaka moja kwa sababu ya dharura ya kibinadamu au faida kubwa ya umma
  • Walioingia kutoka Cuba/Haiti
  • Baadhi ya wageni waliopigwa au wenzi wao au watoto
  • Baadhi ya waathiriwa wa aina kali ya usafirishaji haramu wa binadamu, ikijumuisha watu wenye visa ya “T” au “U”
  • Wakazi halali kwa mujibu wa Makubaliano ya Ushirika Huru na Nchi Zilizoshirikishwa za Mikronesia, Jamhuri ya Visiwa vya Marshall na Jamhuri ya Palau.

Ikiwa mwombaji hajatimiza matakwa ya uraia au uhamiaji wakati anapojaza ombi, familia inaweza kujaza ombi la kupokea msaada fulani kutoka kwa serikali ikiwa:

Mzazi au mlezi halali wa mtoto mdogo ambaye ni raia wa Marekani au mgeni anayestahili hutuma ombi la msaada kwa niaba ya mtoto mdogo, mradi wanaishi katika nyumba moja. Mzazi au mlezi halali lazima atume ombi kama mwombaji mwenza, na mtoto mdogo lazima awe chini ya miaka 18 wakati janga lilitokea.

Watu wote walioathiriwa na janga kubwa, haijalishi uraia wao au hali yao ya uhamiaji, wanaweza kupokea msaada wa ushauri wa jinsi ya kukabiliana na janga, huduma za kisheria zinazohusiana na janga, kushughulikia hali za janga, lishe ya ziada wakati wa janga, na misaada mingine isiyo ya kipesa inayotolewa wakati wa dharura ya janga. Inatia ndani matibabu, makazi, chakula na maji.

Vyanzo vya Misaada

alert - warning

Mtu anapaswa kwenda kwa maofisa wa uhamiaji ili wamsaidie kujua ikiwa ametimiza matakwa ya uhamiaji yatakayomwezesha kupokea msaada wa FEMA wakati wa majanga.

Pia, mashirika mengine ya kujitolea hutoa misaada bila kujali hali ya uraia au uhamiaji.

Watu wote walioathiriwa na janga kubwa, haijalishi uraia wao au hali yao ya uhamiaji, wanaweza kupokea msaada wa ushauri wa jinsi ya kukabiliana na janga, huduma za kisheria zinazohusiana na janga, kushughulikia hali za janga, lishe ya ziada wakati wa janga na misaada mingine isiyo ya kipesa inayotolewa wakati wa dharura ya janga. Inatia ndani matibabu, makazi, chakula na maji.

Tembelea Ukurasa wa Mashirika ya Kujitolea ili upate habari zaidi.

Ilisasishwa mara ya mwisho