Msaada wa Makazi na Mahitaji Mengineyo

alert - info

Taarifa kwenye ukurasa huu haionyeshi masasisho ya Usaidizi wa Mtu Binafsi kwa majanga yaliyotangazwa mnamo au baada ya tarehe 22 Machi, 2024.

Jifunze zaidi kuhusu kile kinachopatikana sasa.

FEMA husaidia watu binafsi na familia ambazo nyumba zao ziliharibiwa sana na majanga yaliyotangazwa na rais. Tunaweza kusaidia na mahitaji mengine ya msaada, kama vile mahitaji ya utunzaji wa watoto yaliyosababishwa na janga, gharama za matibabu ya janga au vitu muhimu vya usafi.

FEMA haitoi msaada kwa biashara ndogo ndogo zilizoathiriwa na janga. Mshirika wetu, Usimamizi wa Biashara Ndogo (SBA), hutoa mikopo ya riba nafuu kwa uharibifu wa biashara. Pia, hatutoi msaada wa makazi kwa nyumba zisizo za msingi, msaada ni wa nyumba za msingi pekee.

Msaada wa FEMA unashughulikia

Familia

Msaada wa Mahitaji Mengineyo

FEMA inaweza kuandaa Msaada wa bidhaa ambazo hazijalipiwa na bima kwa wamiliki wa nyumba na wapangaji. 

Huwezi kupokea Msaada kutoka kwa kampuni yako ya bima na pia FEMA kwa uharibifu uleule. Kufanya hivyo ni kuandaa faida maradufu na udanganyifu haramu wa bima.

Wasilisha Ombi la Msaada wa FEMA kwa DisasterAssistance.gov

External Link Arrow

Familia

Aina zifuatazo za Msaada zinaweza kutolewa na Mpango wa Watu Binafsi na Familia ya FEMA.

  • Msaada wa Makazi ya Muda: Msaada wa kifedha kwa wamiliki wa nyumba au wapangaji ili kukodisha mahali pa kuishi kwa muda ikiwa nyumba yako haiwezi kukaliwa kwa sababu ya janga, na huna bima ya makazi ya muda. Ikiwa hakuna nyumba za kukodisha zinazopatikana, kama njia ya mwisho, kitengo cha makazi cha serikali kinaweza kutumiwa katika baadhi ya maeneo.
  • Urejeshaji wa Gharama za Mahali pa Kukaa: Urejeshaji wa gharama za hoteli kwa wamiliki wa nyumba au wapangaji kwa vipindi vifupi vya wakati kwa sababu ya kutofikiwa au kukatika kwa huduma, ikiwa hailipiwi na bima au programu nyingine yoyote.
  • Ukarabati wa Nyumba: Msaada wa kifedha kwa wamiliki wa nyumba ili kurekebisha uharibifu uliosababishwa na janga kwenye makazi yao ya msingi, wakati uharibifu huo haujagharamiwa na bima, ili kufanya nyumba iwe salama, safi, na kufaa kukaliwa. Msaada huu unaweza kujumuisha fedha za hatua za kupunguza hatari, kama vile paa, tanuri, kipasha-joto cha maji, au upunguzaji wa paneli kuu za umeme, ili kusaidia kupunguza kiasi cha uharibifu wa nyumba katika majanga yajayo, ikiwa vitu hivyo viliharibiwa na janga.

    Tazama Karatasi ya Ithibati ya Upunguzaji wa Hatari Chini ya Mpango wa Watu Binafsi na Familia.
  • Kubadilisha Nyumba: Msaada wa kifedha kwa wamiliki wa nyumba ili kusaidia kubadilisha nyumba zao zilizoharibiwa katika janga, wakati uharibifu haujagharimiwa na bima.
  • Ujenzi wa Makazi ya Kudumu: Msaada wa moja kwa moja au wa kifedha kwa ajili ya ujenzi au ukarabati wa nyumba. Aina hii ya Msaada hutokea tu katika matukio fulani ya kipekee ambapo hakuna aina nyingine ya Msaada wa makazi inawezekana.

Msaada wa Mahitaji Mengineyo

Msaada wa kifedha unapatikana kwa gharama za lazima na mahitaji makubwa yaliyosababishwa moja kwa moja na janga, ikijumuisha:

  • Gharama za utunzaji wa watoto
  • Gharama za matibabu na meno
    • FEMA inaweza kutoa Msaada wa utegemezo na vifaa vya kunyonyeshea chini ya Msaada wa Kimatibabu na Meno wakati mwombaji atakapoandaa hati sahihi za uthibitisho (Taarifa iliyoandikwa na kutiwa sahihi kutoka kwa mhudumu wa afya inayothibitisha uhitaji wa vifaa vya matibabu kabla ya janga.)
  • Mazishi na gharama za kuzika
  • Uharibifu wa vitu muhimu vya nyumbani (vyombo vya chumba, vifaa); mavazi; zana (nguo maalum au za kinga na vifaa) zinazohitajika kwa kazi yako; vifaa vya lazima vya elimu (kompyuta, vitabu vya shule, vifaa)
  • Mafuta kwa ajili ya chanzo kikuu cha joto (mafuta ya kupasha joto, gesi)
  • Vifaa vya usafi (kifyonza vumbi kinachotumia maji/kisichotumia maji, kiondoa unyevunyevu)
  • Uharibifu wa gari ya msingi
  • Gharama za kuhamisha na kuhifadhi zilizosababishwa na janga. Hii ni kuhamisha na kuhifadhi bidhaa muhimu za nyumbani ili kuzuia uharibifu zaidi, kama vile ukarabati unaoendelea, na kurejesha mali kwenye makazi ya msingi ya mwombaji.
  • Gharama nyingine za lazima au mahitaji makubwa kama ilivyobainishwa na FEMA
alert - info

Kwa maelezo ya ziada kuhusu Msaada wa Mahitaji Mengine, tafadhali tembelea Sura ya 3, Sehemu ya VI katika Mpango wa Msaada wa Mtu Binafsi na Mwongozo wa Sera (IAPPG).

Msaada wa Mahitaji Muhimu

Iwapo Msaada wa Mahitaji Muhimu (CNA) umeombwa na kuidhinishwa kwa ajili ya janga lililotangazwa na mwombaji anakidhi matakwa ya kustahili, anaweza kupokea Msaada wa kifedha kwa mahitaji yao ya haraka na muhimu huku akihamishwa kwa muda kutoka kwa makazi yake ya msingi.

Vitu vya kuokoa maisha na kudumisha maisha vikiwa ni pamoja na, lakini sio tu:

  • Maji
  • Chakula
  • Huduma ya kwanza
  • Dawa
  • Chakula cha watoto wachanga
  • Msaada na vifaa vya kunyonyeshea
  • Nepi
  • Vitu vya usafi wa kibinafsi
  • Mafuta ya usafiri
Ilisasishwa mara ya mwisho