Shirika la FEMA Linatumia Lugha Yako

Release Date Release Number
014
Release Date:
Oktoba 25, 2021

NEW YORK – Shirika la FEMA linatoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa ili kufikia na kuwasiliana na waathiriwa wa mikasa wasiojua au wanaojua Kiingerza kidogo. Shirika la FEMA vilevile lina wafanyakazi na teknolojia za kuwasaidia viziwi, walio na ugumu wa kusikia, au wasioona vizuri.

Tafsiri zinajikita katika lugha zilizobainishwa na Hesabu ya Watu Marekani na tafiti nyingine.  

Katika jiji la New York, huduma za FEMA za tafsiri za maandishi huwezesha ujumbe kuwasilishwa katika lugha 25: Kialbania, Kiarabu, Kibengali, Kiburma, Kichina Sahili, Kifaransa, Kigiriki, Kigujarati, Kikrioli cha Haiti, Kiyahudi, Kihindi, Kiitaliano, Kijapani, Kirundi, Kikorea, Kimalaysia, Kipolandi, Kireno, Kirusi, Kihispania, Kiswahili, Kitagalogi, Kiurdu, Kivietinamu na Kiyidi. Lugha zaidi zaweza kuongezwa ikibidi.   

Kuhusu taarifa za Kimbunga Ida katika jiji la New York, shirika la Fema vilevile huchapisha taarifa zake rasmi na muhimu katika lugha 25 kwenye tovuti yake, fema.gov. Huduma ya FEMA ya ukalimani kwa njia ya simu huwezesha mawasiliano kwa lugha 117.

Unapopiga Simu ya FEMA ya Usaidizi kupitia 800-621-3362, wale ambao wanatumia huduma ya relay ya video, huduma ya simu ya maandishi (captioned telephone) au huduma nyingine, wape FEMA nambari ya huduma hiyo. Wahudumu katika simu ya usaidizi wanapatikana kuanzia saa mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa moja jioni (7 p.m.) kila siku. Bonyeza 2 kupata huduma kwa lugha ya Kihispania au 3 kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.  

Unaweza kutembelea Kituo cha Kutoa Ufadhili na kukutana ana kwa ana na wafanyakazi wa FEMA na wawakilishi wa taasisi za kitaifa na jimbo ambao wanaweza kukupa habari zaidi kuhusu ufadhili wa mikasa. Wafanyakazi wa FEMA wamefunzwa kutumia huduma za ukalimani.

Mwathiriwa wa mkasa aliye na uwezo mdogo wa kutumia Kiingereza ataonyeshwa kielelezo cha kutambua lugha chenye maneno “Ninazungumza … ” katika lugha 69. Mwathiriwa wa mkasa anaweza kuashiria lugha ambayo anaelewa, na mwakilishi wa FEMA anaweza kumuunganisha na mkalimani wa lugha hiyo.   

Waathiriwa wa mkasa ambao wanaishi katika kaunti tisa zifuatazo wanahimizwa kutuma maombi ya ufadhili wa mikasa: Bronx, Dutchess, Kings, Nassau, Queens, Richland, Rockland, Suffolk na Westchester.

Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida jijini New York, tembelea fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho