Jumatatu ndio Makataa ya Wakazi wa Vermont Kutuma Ombi la Usaidizi wa Serikali

Release Date Release Number
023
Release Date:
Novemba 22, 2024

Wakazi wa Vermont walioathiriwa na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi, na maporomoko ya matope wana hadi saa nne usiku (10 p.m)Jumatatu, Novemba 25 ili kutuma maombi ya msaada wa majanga ya serikali, ambayo inaweza kujumuisha ruzuku za FEMA za kukarabati nyumba na kubadilisha mali. 

Kwa dhoruba zilizofanyika Julai 9-11, wakazi katika kaunti zilizoteuliwa za Addison, Caledonia, Chittenden, Essex, Lamoille, Orleans na Washington wanastahili kutuma maombi. Kwa ajili ya dhoruba za Julai 29-31, wale walio katika kaunti zilizoteuliwa za Caledonia, Essex na Orleans wanaweza kutuma maombi. 

Wakazi wa Vermont walioathirika na Dhoruba zote mbili za julai lazima wawasilishe maombi tofauti kwa kila tukio. 

Waliookoka ambao walipata hasara au uharibifu wanapaswa kutuma maombi kwa FEMA hata kama hawana makadirio ya ukarabati au malipo ya bima bado. Ili kuzingatiwa, watu katika maeneo yaliyoathiriwa wanahitaji kusajiliwa katika mfumo kabla ya tarehe ya mwisho. 

Hapa kuna njia tatu za kutuma maombi: 

  • Kupitia mtandao DisasterAssistance.gov
  • Piga Simu ya Msaada ya FEMA kwa 1-800-621-3362. Laini za simu hufanya kazi kutoka saa moja asubuhi (7 a.m) hadi saa nne usiku (10 p.m) (kulingana na saa za eneo lako), siku saba kwa wiki. Msaada unapatikana katika lugha nyingi. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji wa video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo. Kupata video ya jinsi ya kutuma ombi la usaidizi nenda kwa, youtube.com/watch?v= WZGpWI2RCNw
  • Pakua Programu ya Simu ya FEMA

Wale ambao hawajatuma maombi kufikia tarehe ya mwisho na bado wanataka kujiandikisha lazima wawasilishe sababu nzuri ya kwa nini walikosa. Sababu zinaweza kujumuisha: rekodi ya kulazwa hospitalini, ugonjwa, au ulemavu wa mwombaji au mwanafamilia wa karibu; kifo cha mwanafamilia wa karibu; au uthibitisho wa safari ya kibinafsi au ya biashara ambayo ilimweka mwombaji nje ya eneo kwa kipindi chote cha maombi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho