Wakaazi wa Kaunti ya Orleans ambao nyumba zao au mali zao za kibinafsi ziliharibiwa wanaweza kutuma maombi ya msaada wa majanga kwa FEMA. Kaunti za ziada zinaweza kuongezwa baadaye ikiwa serikali itaomba na kuthibitishwa na matokeo ya tathmini zaidi za uharibifu.
Kaunti ya Orleans ni pamoja na kaunti nane ambazo tayari zimeteuliwa kwa Msaada wa Mtu Binafsi: Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Rutland, Washington, Windham na Windsor.
Msaada unaweza kujumuisha ruzuku kwa ajili ya ukarabati wa nyumba na makao ya muda, mikopo ya riba nafuu ili kufidia mali iliyopotea isiyo na bima na programu nyinginezo za kuwasaidia watu binafsi na wamiliki wa biashara kurejelea hali ya kawaida baada ya majanga.
Ili kutuma ombi la msaada, piga simu kwa Laini ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362 kati ya saa moja asubuhi (7 a.m.) na saa tano usiku (11 p.m).; nenda mtandaoni kwa DisasterAssistance.gov; au pakua FEMA App. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.
Kwa habari za hivi punde tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Region 1 katika Twitter twitter.com/FEMARegion1 au ukurasa wa Facebook katika facebook.com/FEMA.
Kwa masasisho kuhusu itikio na msaada wa Vermont, fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont twitter.com/vemvt kwenye Twitter na Facebook facebook.com/vermontemergencymanagement.
FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaotumia lugha mbali mbali wanapatikana.