Kisima kilichoharibiwa, Tanuri au Mfumo wa Maji taka? FEMA Inaweza Kusaidia

Release Date Release Number
006
Release Date:
Julai 23, 2023

WILLISTON, Vt. – Iwapo haupati maji kwa sababu kisima cha kibinafsi au mfumo wa maji taka uliharibiwa, au ikiwa Mfumo au tanuri yako ya HVAC iliharibiwa na mafuriko ya hivi majuzi katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Rutland, Washington, Windham na Windsor, huenda unastahili kupokea msaada wa FEMA.

Kwa visima vya kibinafsi, Mifumo ya HVAC, tanuri na mifumo ya maji taka, FEMA inaweza kukulipia gharama ya mtaalamu, fundi aliyeidhinishwa kutembelea nyumba yako na kuandaa makadirio ya ukarabati unaohitajika au kubadilisha mifumo yako iliyoharibiwa na majanga.

FEMA pia inaweza kulipia gharama halisi ya ukarabati au kubadilisha mfumo wako wa maji taka au kisima cha kibinafsi, vitu ambavyo havishughulikiwa na bima.

Iwapo uliomba usaidizi wa FEMA utazungumziwa kuhusu ukaguzi wa nyumba, piga simu kwa nambari ya usaidizi ya FEMA kwa 1-800-621-3362 ikiwa hujazungumziwa na imekuwa zaidi ya siku 7-10. Wakati wa ukaguzi wako, mjulishe mkaguzi wa FEMA kwamba una kisima cha kibinafsi na/au mfumo wa maji taka ambao huenda umeharibika. Ikiwa uharibifu utathibitishwa kuwa ulisababishwa na mafuriko, unaweza kustahili usaidizi wa FEMA.

Ikiwa tayari ukaguzi ulifanywa na uharibifu wa kisima au mfumo wa maji taka haukuripotiwa, piga Simu ya Usaidizi ya FEMA ili kuwasasisha kuhusu uharibifu. Tafadhali dumisha taarifa ya mkandarasi wako, makadirio na risiti. Unaweza kurejelea barua ya uamuzi ya FEMA uliyopokea kwa maelezo zaidi au mwongozo wa rufaa ikiwa uamuzi tayari umefanywa

Ili kujiandikisha kwa usaidizi wa FEMA, piga simu kwa nambari ya usaidizi ya FEMA kwa 1-800-621-3362, nenda mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au upakue FEMA App. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji wa video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi. 

Iwapo unaishi katika kaunti ambayo haijateuliwa na umepata uharibifu, unaweza kupiga simu kwa Nambari ya Usaidizi ya FEMA kwa 1-800-621-3362 ili kutuma maombi na uteuzi wa kaunti yako ukitokea, ombi lako litaanza kushughulikiwa.

FEMA imejitolea kuhakikisha usaidizi wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa maafa au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaozungumza lugha nyingi wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho