FEMA Katika Lugha Yako

Tovuti ya FEMA ina habari na bidhaa katika lugha zingine mbali na Kiingereza.

Waathiriwa wa majanga wanaweza kupata habari zilizotafsiriwa kuhusu jinsi ya kupata msaada wakati wa majanga, kujitayarisha kwa ajili ya dharura, kuchukua hatua, shughuli za baada ya janga, na bima ya mafuriko. Habari hizo zinapatikana katika mifumo mbalimbali na hivyo inaweza kutumwa kidijitali na vilevile kupakuliwa. Vipengele zaidi vitaongezwa mara kwa mara, kwa hivyo, tafadhali tembelea tovuti hii kwa ukawaida.

Graphic
man and woman signing

Maandalizi Yanayofaa

FEMA huandaa huduma kadhaa ili kukidhi mahitaji ya waathiriwa wote wa majanga kutia ndani:

  • Tafsiri
  • Lugha ya Ishara ya Marekani (ASL)
  • Manukuu ya wakati halisi
  • Vifaa vya kusaidia kusikiliza au kusoma
  • Habari katika maandishi ya vipofu (Breli) au chapa kubwa

Omba Huduma

FEMA Huzungumza Lugha Yako

https://www.youtube.com/embed/0VuJUHJO64Q

Tunaandaa msaada na habari katika lugha yako. Piga nambari ya FEMA ya Msaada kwa 800-621-3362:

  • Bonyeza 1 kwa ajili ya Kiingereza
  • Bonyeza 2 kwa ajili ya Kihispania
  • Bonyeza 3 kwa ajili ya lugha zingine

Bonyeza 711 au kwa huduma za usambazaji video zilizopo.

Fahamiana na Rasilimali Zetu

Jifunze kuhusu programu za kuandaa msaada wa majanga na matakwa ya kustahili ya watu, familia, jimbo, mwenyeji, nchi za lugha fulani au serikali za majimbo na mashirika ya kibinafsi yasiyo ya kibiashara.

Pakua rasilimali za Njia tofauti za Mawasiliano kama vile michoro, trakti, matangazo, video na vibonzo katika lugha mbalimbali ili uweze kushiriki na wengine habari muhimu za majanga kabla, wakati na baada ya janga.

Tembelea FloodSmart.gov (en español) ili kujifunza kuhusu bima ya mafuriko, hatari na gharama, na maeneo na ramani na kujitayarisha kwa ajili ya janga la mafuriko. Mawakala wanaweza kutumia lugha mbalimbali za rasilimali za janga la mafuriko kwa ajili ya mikutano na wateja wao au kwenye mitandao ya kijamii, tovuti au katika barua-pepe za mauzo.

Shiriki broshua ya FEMA ya msaada baada ya janga pamoja na watu katika jamii yako ili kuwasaidia waelewe aina mbalimbali za misaada ya FEMA inayoweza kupatikana ili kusaidia katika kurudia hali ya kawaida. Broshua hii inapatikana katika lugha 27.

Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kusaidia walio na uhitaji katika janga. Kuna njia nyingi za kusaidia kama vile kutoa mchango wa kifedha, vifaa vinavyohitajika au wakati wako.

Pata miongozo ya msingi kuhusu jinsi ya kuhifadhi vitu vya thamani vya familia yako kama vile picha, vitabu, stakabadhi muhimu na hati baada ya janga.

Video za Lugha ya Ishara ya Marekani

Tuna video katika lugha ya ishara ya Marekani ASL kwenye orodha yetu ya video katikaYouTube zinazoangazia mambo mbalimbali yanayohusiana na kujitayarisha kwa ajili ya janga na usalama.

Tazama Video Zote Kwenye YouTube

External Link Arrow
Ilisasishwa mara ya mwisho