Wiki Mbili Zimesalia kwa Wakazi Vermont Kutuma Maombi ya Msaada wa Serikali

Release Date Release Number
021
Release Date:
Novemba 10, 2024

Wakazi wa Vermont walioathiriwa na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi, na maporomoko ya matope wana wiki mbili za kutuma maombi ya msaada wa majanga ya serikali, ambayo inaweza kujumuisha msaada wa FEMA ili kukarabati nyumba na kurejesha mali au mikopo ya majanga yenye riba nafuu kutoka kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani. Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 25 Novemba 2024.

Kwa dhoruba zilizotokea Julai 9-11, wakazi katika kaunti zilizoteuliwa za Addison, Caledonia, Chittenden, Essex, Lamoille, Orleans na Washington wanastahili kutuma maombi. Kwa dhoruba za Julai 29-31, wale walio katika kaunti zilizoteuliwa za Caledonia, Essex na Orleans wanaweza kutuma maombi. 

Wakazi wa Vermont walioathiriwa na dhoruba zote mbili za Julai lazima watume maombi tofauti kwa kila tukio. 

Walionusurika ambao walipata hasara au uharibifu wanapaswa kutuma maombi kwa FEMA hata kama bado hawana makadirio ya ukarabati au malipo ya bima. Ili kuzingatiwa, watu katika maeneo yaliyoathiriwa wanahitaji kujiandikisha na FEMA ili kuanza mchakato. FEMA itafanya kazi na walionusurika ili kutambua ni habari gani inahitajika ili kubaini ustahilifu.

Kwa wale ambao wangependa kuongea na mtaalamu wa msaada wa majanga ana kwa ana, Vituo viwili vya Msaada wa Majanga vimefunguliwa Vermont. Vituo hivi viko katikaUkumbi wa Mji wa Hinesburg (10632 Route 116) na Kituo cha Usalama wa Umma cha Lyndon katika 366 Main Street. Masaa ni tatu asubuhi (9 a.m) hadi saa kumi na mbili jioni (6 p.m) Jumatatu - Jumamosi. Inafungwa Jumapili.

Wakazi hawahitaji kutembelea DRC ili kutuma maombi kwa FEMA. Hizi ni njia tatu za kutuma maombi: 

  • Kupitia mtandao DisasterAssistance.gov
  • Piga Simu ya Usaidizi ya FEMA kwa 1-800-621-3362. Laini za simu hufanya kazi kutoka saa moja asubuhi (7 a.m) hadi saa nne usiku (10 p.m). (katika saa za eneo lako), siku saba kwa wiki. Usaidizi unapatikana katika lugha nyingi. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo. Kupata video ya jinsi ya kutuma ombi la usaidizi nenda kwa, youtube.com/watch?v= WZGpWI2RCNw..
  • Pakua Programu ya Simu ya FEMA

Kutuma ombi kwa SBA:

  • Tuma maombi mtandaoni na upokee maelezo ya ziada kuhusu msaada wa majanga kwa sba.gov/disaster
  • Piga simu kwa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha SBA kwa (800) 659-2955 kutoka saa mbili asubuhi (8: 00 a.m.) hadi saa mbili usiku (8: 00 p.m. ET) Jumatatu hadi Ijumaa au tuma barua pepe kwa disastercustomerservice@sba.gov kupata maelezo zaidi. 
  • Kwa watu ambao ni viziwi, wasiosikia vizuri, au wenye ulemavu wa kuzungumza, tafadhali piga 7-1-1 ili kupata huduma za mawasiliano ya simu.

Mnamo Oktoba 15, 2024, ilitangazwa kuwa pesa ya Mpango wa Mkopo wa Majanga ya SBA zimetumika kikamilifu. Ingawa hakuna mikopo mipya ya SBA ya Majanga inayoweza kutolewa hadi Bunge itakapoidhinisha ufadhili wa ziada, SBA inasalia kujitolea kusaidia manusura wa majanga. Maombi yataendelea kukubaliwa na kushughulikiwa ili kuhakikisha kuwa watu binafsi na biashara ziko tayari kupokea usaidizi mara ufadhili utakapopatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho