Kituo cha Msaada wa Majanga Newport Kimeratibiwa Kufungwa Novemba 9

Release Date Release Number
19
Release Date:
Novemba 6, 2024

Kituo cha Msaada wa Majanga (DRC) kilicho katika Jengo la Manispaa ya Jiji la Newport katika 222 Main Street kimeratibiwa kufungwa kabisa saa kumi na mbili jioni, Jumamosi, Novemba 9. Saa za kituo hadi wakati huo ni saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

Kituo hicho kilifunguliwa kwa ajili ya wakazi walioathiriwa na dhoruba na mafuriko yaliyotokea Julai 9-11 na Julai 29-31 na ambao walitaka kuzungumza na FEMA na wataalamu wengine wa kukabiliana na majanga ana kwa ana.

Wakazi hawahitaji kutembelea DRC ili kutuma maombi ya msaada wa FEMA. Njia zingine za kujiandikisha kabla ya tarehe ya mwisho ya Novemba 25 ni pamoja na:

  • Kupitia mtandao DisasterAssistance.gov
  • Kupitia FEMA mobile app
  • Piga simu ya usaidizi ya FEMA kwa 800-621-3362.Usaidizi unapatikana katika lugha nyingi. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine ya usambazaji, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapopiga simu. Laini za simu hufanya kazi kutoka saa moja asubuhi hadi saa tano usiku. siku saba kwa wiki.                         

Baada ya tarehe ya mwisho, wataalamu wa FEMA bado watapatikana ili kuwasaidia waombaji. Wale ambao tayari wametuma maombi kwa FEMA, wanaweza kuuliza maswali, kusasisha maelezo ya mawasiliano na maombi na kupata ushauri wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa FEMA kwa kupiga simu ya usaidizi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho