Wapangaji Wanaweza Kutuma Ombi la Msaada wa FEMA

Release Date Release Number
007
Release Date:
Julai 24, 2023

WILLISTON, Vt.– Wapangaji katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Rutland, Washington, Windham na Windsor ambao nyumba na mali zao ziliharibiwa na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya udongo wanaweza kutuma maombi ya msaada wa Majanga ya FEMA.

Msaada kwa Mtu Binafsi ya FEMA inapatikana kwa wapangaji, ikijumuisha wanafunzi, pamoja na wamiliki wa nyumba. Misaada ya serikali inaweza kusaidia kulipia makazi ya muda. Msaada wa kwanza wa kukodisha ni wa kipindi cha mwezi mmoja au miezi miwili na inaweza kukaguliwa kwa msaada zaidi.

Wapangaji wanaweza pia kustahili kupata msaada chini ya mpango wa Usaidizi wa Mahitaji Mengine ya FEMA kwa ajili ya kuharibika kwa mali muhimu ya kibinafsi isiyo na bima na gharama zingine zinazohusiana na majanga. Hizi zinaweza kujumuisha:

  • Kubadilisha au ukarabati wa mali muhimu ya kibinafsi, kama vile fanicha, vifaa, nguo, vitabu vya kiada au vifaa vya shule.
  • Kubadilisha au ukarabati wa zana na vifaa vingine vinavyohusiana na kazi vinavyohitajika na waliojiajiri.
  • Ikiwa gari lako la msingi liliharibiwa na dhoruba na halitumiki tena (na gari linatii matakwa ya usajili wa serikali na bima) FEMA inaweza kukusaidia. Sio uharibifu wote unaoshughulikiwa, kwa hivyo wasiliana na FEMA ili kuona ikiwa gari lako linastahili.
  • Gharama ya matibabu isiyoshughulikiwa na bima au unayojilipia mwenyewe, meno, malezi ya watoto, kuhamisha na kuhifadhi.

Unaweza kutuma maombi kwa FEMA ili kupata msaada wa serikali kwa kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga.

Huhitaji kutembelea kituo cha msaada ili kutuma maombi ya usaidizi wa FEMA. Kutuma maombi bila kutembelea kituo, nenda kwenye mtandao DisasterAssistance.gov  piga simu kwa laini ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362 kutoka saa moja asubuhi (7:00 a.m) hadi saa tano usiku (11:00 p.m) Masaa ya Mashariki siku saba kwa wiki, au tumia FEMA mobile app. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari ya huduma hio. Msaada unapatika kwa lugha nyingi.

Ikiwa unaishi katika kaunti ambayo haijateuliwa na umepata uharibifu unaweza kupiga Simu kwa laini ya Msaada ya FEMA kwa 1-800-621-3362 ili kutuma ombi na uteuzi wa kaunti yako ukitokea, ombi lako litaanza kushughulikiwa.

Vituo hivyo vinaweza kutumiwa na watu wenye ulemavu kwa urahisi na vina vifaa vya teknolojia saidizi. Manusura wanaohitaji makao ya kuridhisha au mkalimani wa lugha ya ishara wanaweza kupiga simu kwa 833-285-7448 (bonyeza 2 kwa Kihispania).

Wawakilishi kutoka Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani (SBA) pia watakuwa katika vituo hivyo kueleza jinsi ya kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu ya SBA kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara na mashirika yasiyo ya kibiashara ya kibinafsi, na kutoa maelezo kuhusu kujenga upya ili kufanya nyumba zistahimili majanga zaidi.

Wapangaji pia wanaweza kukopa hadi $40,000 kutoka SBA ili kubadilisha mali ya kibinafsi iliyoharibika au kuharibiwa kama vile nguo, fanicha, vifaa au magari. Inapendekezwa watume ombi la msaada wa FEMA kabla ya kutuma ombi kwa SBA, lakini si lazima.

Kwa habari ya hivi karibuni tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Mkoa wa 1 kwenye Twitter katika twitter.com/FEMARegion1 au kwenye ukurasa wa Facebook facebook.com/FEMA.

Kwa masasisho kuhusu Itikio na Urejeshaji wa Vermont, fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont twitter.com/vemvt kwenye Twitter na Facebook facebook.com/vermontemergencymanagement

FEMA imejitolea kuhakikisha usaidizi wa maafa unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wa lugha nyingi wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho