Zaidi ya dola milioni 101.2 za usaidizi wa serikali na jimbo sasa zimeidhinishwa kwa wakazi wa Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles walioathiriwa na mafuriko ya Julai 25-28. Takriban wafanyakazi 200 wa serikali kutoka kote nchini wamesalia kazini huko Missouri wakisaidia kukabiliana na athari za mafuriko.
Kuanzia Okt. 13, 2022:
- FEMA imeidhinisha dola milioni 38.2 kwa usaidizi kwa watu binafsi na familia, ikijumuisha usaidizi wa kukodisha kwa wamiliki wa nyumba na wapangaji.
- Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani (SBA) imeidhinisha dola milioni 28.3 za mikopo ya majanga kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji na wafanyabiashara 879.
- Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Mafuriko umepokea madai 602 na kulipa dola milioni 34.7.
"Tumefurahi kuona kwamba usaidizi wa kifedha unaohitajika sana unawafikia watu katika eneo la St. Louis ili kuwasaidia kutokana na mafuriko ya kihistoria," Mkurugenzi wa Usimamizi wa Dharura wa Jimbo la Missouri Jim Remillard alisema. "Wakazi wa Missouri wameongezewa muda hadi Novemba 7, 2022 ili kutuma maombi ya usaidizi. Tunataka kila mtu ajue kwamba usaidizi wa FEMA bado unapatikana, ikijumuisha kwa ajili ya kurekebisha nyumba na mahitaji ya muda ya makazi, na gharama nyinginezo. Msaada huu unapatikana kwa wapangaji na pia wamiliki wa nyumba. Tunawahimiza watu katika St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles ambao waliathiriwa moja kwa moja na mafuriko ya Julai kutuma maombi kwa FEMA, mtandaoni, kwa simu au kutumia programu ya FEMA.”
"FEMA ni sehemu moja tu ya mchakato wa kusaidia na majanga. Kwa kufanya kazi kwa karibu na Jimbo la Missouri, maafisa waliochaguliwa katika eneo, mashirika yasiyo ya kibiashara na mashirika mengine ya serikali, tumeweza kuleta usaidizi kwa haraka mikononi mwa waathirika wa mafuriko ya Julai. Usaidizi huu utasaidia kuanza kurejea hali ya kawaida,” alisema DuWayne Tewes, Afisa Mratibu wa Shirikisho la FEMA. "Huu ni mwanzo tu. Tunajua kuna kazi nyingi ya kufanya. Kwa hivyo tunawatia moyo wale ambao wameathiriwa, lakini bado hawajatuma ombi la usaidizi wa FEMA, wafanye hivyo kabla ya Novemba 7. Tunataka kuhakikisha kwamba kila mtu anayestahili anasajiliwa.” Tewes aliongeza.
Watu walioathiriwa na janga katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis, na Kaunti ya St. Charles wana njia tatu za kutuma maombi na kuwasiliana na FEMA:
- Piga simu: 1-800-621-FEMA (3362)
- Enda kwenye mtandao: DisasterAssistance.gov
- Kituo chochote cha Msaada wa Majanga
FEMA inaendelea kuendesha Vituo vya Msaada wa Majanga katika maeneo yaliyoathiriwa. Vituo vya msaada huwaruhusu walionusurika kukutana ana kwa ana na FEMA na SBA. Vituo hivi vimehudumia zaidi ya manusura 5,700 na vinaendelea kusaidia wanaohitaji msaada.
Timu za FEMA za Msaada kwa Walionusurika Majanga (DSA) zilitembelea maeneo yaliyoathiriwa na maafa katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles. Wafanyakazi wa DSA walikutana ana kwa ana na wapangaji na wamiliki wa nyumba ili kuwasaidia kutuma maombi na FEMA na kutambua kwa haraka na kushughulikia mahitaji ya haraka na yanayojitokeza. FEMA ilituma timu za DSA nyumba kwa nyumba kukutana na manusura ambao ni vigumu kuwafikia wanakoishi ili kusaidia kuendeleza mchakato wa msaada. Timu za DSA zimegonga zaidi ya milango 30,000 na kuwa na mwingiliano zaidi ya 14,500 na walionusurika.
Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.
Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.
Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.