Wakazi wa Vermont walioathiriwa na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi, na maporomoko ya matope wana hadi saa nne usiku (10 p.m)Jumatatu, Novemba 25 ili kutuma maombi ya msaada wa majanga ya serikali, ambayo inaweza kujumuisha ruzuku za FEMA za kukarabati nyumba na kubadilisha mali.
News, Media & Events: Vermont
Preparedness Tips
Press Releases and Fact Sheets
Vituo vya Msaada wa Majanga(DRC) vilivyo Hinesburg Town Hall (Route 10632) na Lyndon Public Safety Facility (316 Main Street) vimepangwa kufungwa kabisa saa kumi na mbili jioni (6 p.m) Jumamosi, Novemba. 23. Masaa ya kazi ya vituo hadi wakati huo ni tatu asubuhi (9 a.m) hadi kumi na mbili jioni (6 p.m).
Ingawa makataa ya kujiandikisha na FEMA yalipita Novemba 25 kwa wale walioathiriwa na dhoruba kali za Julai, wawakilishi wa wakala bado wanapatikana ili kujibu maswali na kusaidia wakazi wa Vermont kukamilisha maombi yao. Wakala pia inawahimiza waombaji kudumisha mawasiliano, hasa ikiwa kuna mabadiliko ya anwani au masasisho mengine kwa maombi yao.