Vituo vya Msaada wa Majanga(DRC) vilivyo Hinesburg Town Hall (Route 10632) na Lyndon Public Safety Facility (316 Main Street) vimepangwa kufungwa kabisa saa kumi na mbili jioni (6 p.m) Jumamosi, Novemba. 23. Masaa ya kazi ya vituo hadi wakati huo ni tatu asubuhi (9 a.m) hadi kumi na mbili jioni (6 p.m).
Vituo hivyo vilifunguliwa kwa ajili ya wakazi walioathiriwa na dhoruba na mafuriko Yaliyotokea Julai 9-11 na Julai 29-31 na ambao walitaka kuzungumza NA FEMA na wataalamu wengine wa msaada wa majanga ana kwa ana.
Wakazi hawahitaji kutembelea DRC kuomba msaada wa FEMA. Njia nyingine za kujiandikisha kabla ya Novemba 25 tarehe ya mwisho ni pamoja na:
- Mtandao kupitia DisasterAssistance.gov
- Kutumia Programu ya simu ya fema
- Kupiga Simu ya msaada ya FEMA katika 800-621-3362. Msaada unapatikana katika lugha nyingi. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine ya mawasiliano, pea fema nambari yako ya huduma hiyo unapopiga simu. Laini za simu hufanya kazi kutoka saa moja asubuhi hadi tano usiku ( 7 a.m. to 11 p.m.) siku saba kwa wiki.
Baada ya tarehe ya mwisho, wataalam WA FEMA bado watapatikana kusaidia walio tuma maombi. Wale ambao tayari wametuma maombi kwa FEMA, wanaweza kuuliza maswali, kusasisha habari ya mawasiliano na maombi na kupata ushauri kuhusu kukata rufaa uamuzi wa FEMA kwa kupiga simu ya msaada.