Makataa ya FEMA Yalipita lakini Msaada Bado Unapatikana

Release Date Release Number
024
Release Date:
Novemba 26, 2024

Ingawa makataa ya kujiandikisha na FEMA yalipita Novemba 25 kwa wale walioathiriwa na dhoruba kali za Julai, wawakilishi wa wakala bado wanapatikana ili kujibu maswali na kusaidia wakazi wa Vermont kukamilisha maombi yao. Wakala pia inawahimiza waombaji kudumisha mawasiliano, hasa ikiwa kuna mabadiliko ya anwani au masasisho mengine kwa maombi yao. 

Ili kusasisha ombi lako au kupata majibu ya maswali, piga simu ya msaada ya FEMA kwa 1-800-621-3362. Laini za simu hufanya kazi kutoka saa moja asubuhi (7 a.m) hadi saa nne usiku (10 p.m) (kulingana na saa za eneo lako), siku saba kwa wiki. Msaada unapatikana katika lugha nyingi. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji wa video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo. 

Wakazi wa Vermont walistahili kutuma maombi mawili tofauti ya majanga. Ya kwanza ilifanyika Julai 9-11 katika kaunti zilizoteuliwa za Addison, Caledonia, Chittenden, Essex, Lamoille, Orleans Na Washington. Tukio la pili lilitokea Julai 29-31 katika kaunti zilizoteuliwa za Caledonia, Essex na Orleans

Wakazi wa Vermont walioathirika na Dhoruba zote mbili za Julai walihitajika kuwasilisha maombi tofauti kwa kila tukio. 

Wale ambao hawajatuma maombi kufikia tarehe ya mwisho na bado wanataka kujiandikisha lazima wawasilishe sababu nzuri ya kwa nini walikosa. Sababu zinaweza kujumuisha: rekodi ya kulazwa hospitalini, ugonjwa, au ulemavu wa mwombaji au mwanafamilia wa karibu; kifo cha mwanafamilia wa karibu; au uthibitisho wa safari ya kibinafsi au ya biashara ambayo ilimweka mwombaji nje ya eneo kwa kipindi chote cha maombi.

Watalamu wa msaada wa FEMA wanaendelea kufuatilia na waombaji ili kuhakikisha wanapokea msaada wote ambao wanastahili. Kufikia sasa, kati ya jumla ya waombaji 2,282 waliojiandisha kwa ajili ya tukio la julai 9-11, FEMA imefuatilia na 1,706 na kupitisha zadi ya $1.4 milioni. Kwa tukio la julai 29-31, wataalamu waliwasiliana na wasajili 245 kati ya jumla ya 313 na kupitisha ziada ya $220,000. 

Kufikia Novemba 25, wakazi wa Vermont walioathiriwa na mafuriko ya Julai wamepokea msaada ufuatao: 

  • Kwa kipindi cha Julai 9-11, zaidi ya million 9.1 imeidhinishwa. 
    • Dola 5,395,139 kwa ajili ya Msaada wa Makazi 
    • Dola 3 3,253,144 kwa ajili ya Mahitaji Mengine
    • Dola 505,500 kwa ajili ya mikopo ya majanga yenye riba ya chini kutoka kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani   

          (SBA)

  • Kwa kipindi cha Julai 29-31, zaidi ya dola millioni 1.2 zimeidhinishwa. 
    • Dola 728,185 kwa ajili ya Msaada wa Makazi
    • Dola 477,183 kwa ajili ya Mahitaji Mengine
    • Dola 31,200 kwa ajili mikopo ya majanga yenye riba ya chini kutoka SBA
Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho