Kituo cha Muda cha Kutoa Misaada ya Mikasa cha FEMA Kuletwa Bronx

Release Date:
Oktoba 27, 2021

Kituo cha muda cha kutoa misaada ya mikasa cha FEMA kitakuwa katika Kaunti ya Bronx kati ya Oktoba 29 na Novemba 1 kuwasaidia waathiriwa wa Kimbunga Ida kutuma maombi ya ufadhili kutoka kwa FEMA na kujibiwa maswali yao.

Waathiriwa wanashauriwa kutembelea kituo hiki cha muda na kukutana na wafanyakazi wa FEMA na wawakilishi wa mashirika mengine ya kitaifa na jimbo. Aidha wanaweza kusaidiwa kupakia stakabadhi zao mtandaoni.  Wawakilishi wa Usimamizi wa Biashara Ndogo Ndogo Marekani (SBA) watakuwepo pia kueleza namna ya kufanya maombi ya kupata mikopo ya riba za chini kugharamia mikasa kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, wafanyabiashara na mashirika binafsi yasiyo ya kibiashara.  

Kituo hiki cha muda Kitakuwa katika:  

Kaunti ya Bronx Saa 3 asubuhi (9 a.m.) hadi saa 11 jioni (5 p.m.)

Aileen B. Recreational Complex katika Pelham Bay Park

Middletown Road and Stadium Avenue

Bronx, NY 10465

Ijumaa, Okt. 29, Jumamosi, Okt. 30 na Jumatatu, Nov. 1

Waathiriwa hawalazimiki kutembelea kituo cha misaada ili waweze kusaidiwa. Wanaweza kutuma maombi ya usaidizi kwa njia ya mtandao kupitia DisasterAssistance.gov, kutumia App ya FEMA ya kwenye simu au kupiga Simu ya FEMA ya Usaidizi kupitia 800-621-3362. Ikiwa unatumia huduma ya relay ya video, huduma ya simu ya maandishi (captioned telephone) au huduma nyingine, wape FEMA nambari ya huduma hiyo. Wahudumu katika laini za usaidizi wanapatikana kuanzia saa mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa moja jioni (7 p.m.) kila siku. Bonyeza 2 kupata huduma kwa lugha ya Kihispania au 3 kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.  

Makataa ya kutuma maombi ya ufadhili wa mikasa wa FEMA ni Jumatatu, Disemba 6.

Kwa taarifa rasmi kuhusu juhudi za kutoa misaada Jijini New York, tembelea fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa za FEMA kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho