Vituo vya Msaada wa Majanga kwa ajili ya dhoruba na mafuriko yaliyotokea Julai 11-13 na Julai 29-31 vitafungwa Siku ya Uchaguzi, Jumanne, Novemba 5.
Vituo hivi viko katika Jengo la Manispaa ya Newport (222 Main St) na katika Kituo cha Usalama wa Umma cha Lyndon (316 Main St).
Kwa sababu kituo katika Jumba la Mji wa Hinesburg ( 10632 Route 116) kitatumika kama eneo la kupiga kura, kitafungwa Jumatatu, Novemba 4 hadi Jumatano, Novemba 6.
Vituo vya Msaada wa Majanga katika Newport na Lyndon vitafunguliwa tena Jumatano saa tatu asubuhi, Nov. 6.
Kituo cha Msaada wa Majanga Hinesburg itafunguliwa tena Alhamisi saa tatu asubuhi, Novemba 7.
Masaa ya Vituo vyote vya Majanga ni Saa tatu asubuhi (9 a.m.) hadi saa kumi na mbili jioni (6 p.m.) Jumatatu – Jumamosi.
Wakazi walioathiriwa na mafuriko hawahitaji kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga ili kutuma maombi au kupokea usaidizi wa FEMA. Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 25 Novemba 2024.
Njia tatu za kutuma maombi ni pamoja na:
- Kupitia mtandao DisasterAssistance.gov
- Kupitia FEMA mobile app
- Piga Simu ya Usaidizi ya FEMA kwa 1-800-621-3362. Laini za simu hufanya kazi kutoka saa moja asubuhi (7 a.m) hadi saa nne usiku (10 p.m) (kulingana na saa za eneo lako), siku saba kwa wiki. Usaidizi unapatikana katika lugha nyingi. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji wa video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo. Kupata video ya jinsi ya kutuma ombi la usaidizi nenda kwa, youtube.com/watch?v= WZGpWI2RCNw.