Kituo cha Msaada wa Majanga kilicho Ferguson Kitafungwa Wiki Ijayo

Release Date Release Number
20
Release Date:
Oktoba 14, 2022

Kituo cha Msaada wa Majanga katika Kaunti ya St. Louis kitafungwa siku ya Jumanne, Oktoba 18 na kufunguliwa tena Jumatano, Oktoba 19 saa mbili asubuhi (8am). Kituo kitafungwa kabisa Ijumaa, Oktoba 21 saa kumi na moja jioni (5pm).

Urban League Empowerment Center

9420 W. Florissant Ave.

Ferguson, MO 63136

Vituo viwili vya Msaada wa Majanga vitasalia wazi ili kuwasaidia walioathirika moja kwa moja na mafuriko na dhoruba kali ya Julai 25-28:

Chuo cha Ranken Technical

Kituo cha Mary Ann Lee Technology

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kwenye kona ya Newstead na Page)

University City Recreation Division

Centennial Commons

7210 Olive Blvd.

University City, MO 63130

Masaa ya vituo vya Msaada:

Jumatatu – Ijumaa, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na mbili jioni (6 p.m).

Jumamosi, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na moja jioni (5 p.m.)

Inafungwa Jumapili

Katika vituo vya msaada wataalamu kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani wanatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao.

  • Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya FEMA ni Oktoba 7.
     
  • Tuma ombi kwa FEMA mtandaoni kupitia DisasterAssistance.gov au piga simu kwa 800-621-FEMA (3362).
     
  • Iwapo unahitaji usaidizi kutuma ombi, FEMA inaweza kukusaidia katika Kituo cha Msaada wa Majanga.
     
  • Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.
  • Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada kupata usaidizi wa ana kwa ana.                                                 

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho