KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA KILICHO FERGUSON KITAFUNGWA WIKI IJAYO [https://www.fema.gov/sw/press-release/20221014/disaster-recovery-center-ferguson-close-next-week] Release Date: Oktoba 14, 2022 Kituo cha Msaada wa Majanga katika Kaunti ya St. Louis kitafungwa siku ya Jumanne, Oktoba 18 na kufunguliwa tena Jumatano, Oktoba 19 saa mbili asubuhi (8am). Kituo kitafungwa kabisa Ijumaa, Oktoba 21 saa kumi na moja jioni (5pm). URBAN LEAGUE EMPOWERMENT CENTER 9420 W. FLORISSANT AVE. FERGUSON, MO 63136 Vituo viwili vya Msaada wa Majanga vitasalia wazi ili kuwasaidia walioathirika moja kwa moja na mafuriko na dhoruba kali ya Julai 25-28: Chuo cha Ranken Technical Kituo cha Mary Ann Lee Technology 1313 N. Newstead Ave. St. Louis, MO 63113 (Kwenye kona ya Newstead na Page) University City Recreation Division Centennial Commons 7210 Olive Blvd. University City, MO 63130 MASAA YA VITUO VYA MSAADA: Jumatatu – Ijumaa, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na mbili jioni (6 p.m). Jumamosi, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na moja jioni (5 p.m.) Inafungwa Jumapili Katika vituo vya msaada wataalamu kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani wanatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao. * Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya FEMA ni Oktoba 7.   * Tuma ombi kwa FEMA mtandaoni kupitia DisasterAssistance.gov [https://www.disasterassistance.gov/] au piga simu kwa 800-621-FEMA (3362).   * Iwapo unahitaji usaidizi kutuma ombi, FEMA inaweza kukusaidia katika Kituo cha Msaada wa Majanga.   * Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa. * Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada kupata usaidizi wa ana kwa ana.                                                  Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA [https://twitter.com/mosema_] na @FEMARegion7 [https://twitter.com/femaregion7]. Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov [https://recovery.mo.gov/] na FEMA.gov/disaster/4665 [https://www.fema.gov/disaster/4665]. _Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi._