ST. LOUIS – Wapangaji na wamiliki wa nyumba katika Kaunti ya St. Louis, Jiji la St. Louis na Kaunti ya St. Charles ambao waliathiriwa na mafuriko Julai 25-28 wanaweza kutuma maombi ya usaidizi wa majanga ya FEMA.
Tuma maombi kwenye mtandao katika DisasterAssistance.gov, kwa kupiga simu 800-621-3362 au kwa kutumia programu ya simu ya FEMA.
Ikiwa unatumia huduma ya relay, kama vile video relay (VRS), simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo.
Kwa mahitaji ambayo hayajashughulikiwa na bima au vyanzo vingine, FEMA inaweza kutoa usaidizi wa pesa kwa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa:
- Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
- Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
- Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
- Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
- Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni
- Ombi moja tu kwa kila familia
FEMA hailipii chakula kilichopotea.
Unapotuma ombi kwa FEMA, uwe na maelezo yafuatayo tayari:
- Nambari ya simu ambayo unaweza kupatikana
- Anwani ya mahali ulipokuwa ukiishi wakati wa mafuriko
- Anwani ya mahali unapoishi sasa
- Nambari ya Ruzuku ya Serikali ya mtu mmoja kati familia
- Orodha ya msingi ya uharibifu na hasara
- Taarifa za benki ukichagua kuwekewa pesa za FEMA moja kwa moja kwenye benki
- Taarifa za Bima ikiwa una bima, ikijumuisha nambari ya sera
Ikiwa una bima ya wamiliki wa nyumba, mpangaji au ya mafuriko, unapaswa kuwasilisha dai haraka iwezekanavyo. FEMA haiwezi kulipia hasara zinazolipiwa na bima. Ikiwa bima yako hailipii gharama zako zote za uharibifu, huenda ukastahili kupokea usaidizi wa nchi.
Piga picha ili kurekodi uharibifu, na uanze kusafisha na kurekebisha ili kuzuia uharibifu zaidi. Kumbuka kuweka risiti kutoka kwa ununuzi wote unaohusiana na kusafisha na kurekebisha.
Kupata video ya jinsi ya kutuma ombi la usaidizi, tembelea youtube.com/watch?v=WZGpWI2RCNw.
Kupata masasisho ya majanga kutoka kwa FEMA, fuata @FEMAregion7 kwenye Twitter, na uwashe arifa za simu. Tembelea tovuti ya majanga kwa fema.gov/disaster/4665.
Kwa masasisho ya majanga kutoka kwa Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Jimbo la Missouri (SEMA), fuata @MOSEMA_ kwenye Twitter, na uwashe arifa za simu. Recovery.MO.gov inaendelea kuwa chanzo cha msingi kwa watu wa Missouri ili kupata taarifa na rasilimali zinazohusiana na majanga kwa urahisi.