Jinsi Programu ya Bima ya Taifa ya Mafuriko Inavyoweza Kuwasaidia Wakazi wa Vermont

Release Date:
Oktoba 16, 2024

Dhoruba za hivi karibuni za Vermont mnamo Julai zinaonyesha kiasi gani mafuriko yanaweza kusababisha madhara. Kukatia bia nyumba yako au biashara kwa sera ya Mpango wa Bima ya Taifa ya Mafuriko kunaweza kukusaidia kujiandaa kwa – kurejea katika hali ya mwanzo – mafuriko ya baadaye.

Mpango wa Bima ya Taifa ya Mafuriko ni nini?

Mpango wa Bima ya Taifa ya Mafuriko (NFIP) unawasidia wamiliki wa mali wapangishaji na wamiliki wa biashara walio katika hatari ya mafuriko ili kupata bima ya mafuriko. Inasimamiwa na FEMA na inapatikana kwa mawakala wengi wa bima wanaowakilisha ama mtandao wa zaidi ya makampuni 50 ya bima au NFIP Direct, NFIP inatoa bima ya mafuriko ili kuwasaidia kurejea haraka katika hali ya mwanzo baada ya tukio la mafuriko. Bima ya mafuriko inatoa kinga ya madhara kwenye nyumba yako au biashara kutokana na mafuriko.

Kwa Wapangishaji, Wamiliki wa Nyumba na Biashara

Sera za NFIP zinapatikana kwa wapangishaji, wamiliki wa nyumba na biashara katika jamii zinazoshiriki katika Bima ya Taifa ya Mafuriko Jamii zinazoshiriki katika NFIP zinafuata mpango wa kupunguza madhara ya mafuriko, mpango unaoweza kujumuisha kuwataka wajenzi kusimika vifaa fulani vya kinga au kuzuia ujenzi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko zaidi. Ili kuona ikiwa jamii yako inakingwa, piga simu Kituo cha Mawasiliano ya Rufaa cha NFIP kwa 800-427-4661 au tembelea FloodReady.Vermont.gov/Find_Funding/Flood_Insurance.

Kwa nini ninahitaji bima ya mafuriko?

Hata kama hauishi katika eneo la "hatari zaidi", nyumba yako bado inaweza kukumbwa na mafuriko – zaidi ya asilimia 20 ya madai ya NFIP yanatoka nje ya maeneo yaliyo na "hatari zaidi". Inchi moja tu ya maji ya mafuriko inaweza kusababisha madhara ya hadi zaidi ya $25,000. Fedha wa FEMA kutoka kwa ruzuku za Msaada wa Watu binafsi na Kaya zitafanya nyumba yako kuwa salama baada ya mafuriko, lakini haziwezi kukinga madhara yote. Chanzo kizuri cha fedha za kurejea katika hali ya mwanzo baada ya mafuriko ni sera ya bima ya mafuriko.

Bima ya Wamiliki wa Nyumba Si Bima ya Mafuriko

Sera za bima ya wamiliki wa nyumba wengi na wapangishaji hazikingi madhara ya mafuriko. Ikiwa sera yako haijumuishi mafuriko, utahitaji bima ya mafuriko ya tofauti ili kukingwa. Sera ya NFIP inakinga hasara za moja kwa moja za jengo lako na mali kupitia aina mbili za bima: bima ya ujenzi na bima ya vilivyomo.

Nyumba yangu imekumbwa na mafuriko. Je, ninaweza kupata bima?

Haijalishi ni mara ngapi nyumba yako, nyumba ya kupangisha au biashara imekumbwa na mafuriko? Ikiwa jamii yako inashiriki katika NFIP, unastahiki kupata bima ya mafuriko.

Ikiwa una bima, wasilisha lalamiko haraka iwezekanavyo. Mpigie simu wakala wako, piga picha ya madhara, na utunze risiti za ukarabati wote. Kwa maelezo zaidi, tembelea www.FloodSmart.gov/How-Do-I-Start-My-Flood-Claim.

Kupata bima sasa hakutakinga madhara ambayo yameshatokea, lakini inaweza kukulinda dhidi ya dhoruba za baadaye. Unaweza kununua bima ya mafuriko wakati wowote. Sera nyingi zina siku 30 za kusubiri baada ya kulipia bima kabla ya kabla ya sera kuanza kutumika.

Ninatumaje maombi ya msaada wa maafa wa FEMA?

Ikiwa una madhara ya mafuriko, FEMA inaweza kusaidia. Ikiwa una bima, hupaswi kusubiri dai lako lishughulikiwe. Wakazi wa Vermont walioathiriwa na matukio mabaya ya hali ya hewa yote ya Julai 2024, wana muda hadi 25 Novemba, 2024, ili kuomba msaada binafsi wa FEMA. Kuna njia nne za kuomba:

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho