WILLISTON, Vt. –Kituo cha Msaada wa Majanga kitafunguliwa huko Barre Julai 27 kusaidia wakaazi wa Vermont walioathiriwa na mafuriko kuanza kurudia hali ya kawaida. DRC ya pamoja, kituo cha muda kilichoanzishwa kwa ushirikiano kati ya Barre, jimbo la Vermont na FEMA, itasaidia waathiriwa kutuma maombi ya usaidizi wa FEMA, kupakia hati na kujibu maswali ana kwa ana.
Kituo cha Barre kinapatikana katika::
Barre Auditorium
16 Auditorium Hill
Barre, VT 05641
Vituo tayari vimefunguliwa katika:
Waterbury Armory
294 Armory Drive
Waterbury, VT 05676
ASA Bloomer Building
88 Merchants Row, Suite 330
Rutland, VT 05701
Kinafunguliwa 7/28:
Flood Brook School
91 Vermont – 11
Londonderry, VT 05148
Zote zinafunguliwa siku 7 kwa wiki, saa mbili asubuhi (8 a.m) hadi saa moja jioni (7 p.m.)
Vituo vyote vinaweza kufikiwa na watu wenye ulemavu na mahitaji ya kutenda, na vina vifaa vya teknolojia ya usaidizi. Ikiwa unahitaji malazi ya kuridhisha au mkalimani wa lugha ya ishara, tafadhali piga simu kwa 1-833-285-7448 (bonyeza 2 kwa Kihispania).
Wawakilishi kutoka Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani (SBA) pia watakuwa kituoni kueleza jinsi ya kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu ya SBA kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara na mashirika yasiyo ya kibiashara ya kibinafsi, na kutoa maelezo kuhusu kujenga upya ili kufanya nyumba zistahimili maafa zaidi.
Huhitaji kutembelea DRC ili kutuma maombi ya msaada wa FEMA. Kutuma ombi bila kutembelea kituo, piga simu kwa nambari ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362, nenda mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au upakue FEMA App. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.
FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa maafa au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wa lugha mbali mbali wanapatikana.