Jihadhari na Ulaghai na Matumizi Mabaya

Release Date Release Number
002
Release Date:
Julai 16, 2023

Majanga huleta wahalifu wanaolenga kuwalaghai wahanga wanaoonekana kuwa walengwa rahisi wa ulaghai huo.

Wahanga wanapaswa kuelewa kuwa matukio ya utapeli na ulaghai yanaweza kutokea wakati wowote. FEMA inawahimiza wahanga kuchukua tahadhari na kuripoti shughuli zozote zinazotiliwa shaka au ulaghai ambao inawezekana unafanywa na wasanii walaghai, wahalifu wanaoiga utambulisho na wahalifu wengineo.

Mtu yeyote anayeshuku tukio la ulaghai au utapeli anapaswa kupiga Simu ya Dharura ya Majanga ya Utapeli ya FEMA kwenda nambari 866-720-5721, TTY piga 711. Nambari isiyolipiwa inapatikana saa 24 kwa siku.

Mbinu za kawaida zinazotumiwa na wasanii walaghai ni pamoja na simu kutoka kwa watu wanaodai wanafanya kazi FEMA. Anayepiga simu anaweza kumwomba nambari ya Usalama wa Jamii ya mhanga, mapato au taarifa za benki.

Kamwe, wahanga hawapaswi kumwamini mtu anayedai kuwa mfanyakazi msaidizi wa majanga akiomba pesa. FEMA haiidhinishi biashara yoyote, bidhaa au huduma, na wafanyakazi wa usaidizi wa majanga wa ndani ya shirikisho hawaombi au kukubali pesa.

Usaidizi wa kushughulikia majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, asili ya kitaifa, jinsia (ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia), mwelekeo wa kingono, umri, ulemavu, ujuzi mdogo wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Ikiwa unaamini kwamba haki zako za kiraia zinakiukwa, unaweza kupiga simu kwa Civil Rights Resource (Nyenzo za Haki za Kiraia) kwenye 833-285-7448.

Kwa taarifa za hivi karibuni tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuatilia akaunti ya FEMA Region 1 kwenye Twittertwitter.com/FEMARegion1 au ukurasa wa Facebook wa FEMA katika facebook.com/FEMA.

Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu uitikiaji na uokoaji wa Vermont, fuatilia Shirika la Usimamizi wa Dharura la Vermont twitter.com/vemvt kwenye Twitter na Facebook facebook.com/vermontemergencymanagement

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho