Kituo cha Msaada wa Majanga Kinafunguliwa katika University City

Release Date Release Number
008
Release Date:
Agosti 25, 2022

Kituo cha msaada wa majanga cha FEMA kitafunguliwa katika University City (Kaunti ya St. Louis) mnamo Ijumaa, Agosti 26 ili kutoa usaidizi wa moja kwa moja kwa watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko na dhoruba kali Julai 25—28.

Wataalamu wa Misaada kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo Marekani watatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao.

Kituo kiko katika:

University City Recreation Center

Centennial Commons

7210 Olive Blvd

University City, MO 63130

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe

Vituo vingine vya msaada vimefunguliwa katika:

KAUNTI YA ST. LOUIS

Kituo cha Hazelwood Civic

8969 Dunn Road

Hazelwood, MO 63042                                   

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe

JIJI LA ST. LOUIS

Chuo cha Ranken Technical

Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kwenye kona ya Newstead na Page)

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe

KAUNTI ST. CHARLES

Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB

1025 Country Club Road

St. Charles, MO 63303

(I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl)

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe

Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.

Kabla ya kutembelea kituo, tuma ombi na FEMA mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au piga simu 800-621-FEMA (3362).

Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada.

  Kwa mahitaji yanayohusiana moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25—28, FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa:

  • Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
  • Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
  • Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
  • Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
  • Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni

Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo:

  • Ombi moja tu kwa kila familia
  • FEMA hailipii chakula kilichopotea au kuharibika

Kisheria. Fema hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine           

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho