KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA KINAFUNGULIWA KATIKA UNIVERSITY CITY [https://www.fema.gov/sw/press-release/20220825/disaster-recovery-center-opening-university-city] Release Date: Agosti 25, 2022 Kituo cha msaada wa majanga cha FEMA kitafunguliwa katika University City (Kaunti ya St. Louis) mnamo IJUMAA, AGOSTI 26 ili kutoa usaidizi wa moja kwa moja kwa watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko na dhoruba kali Julai 25—28. Wataalamu wa Misaada kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo Marekani watatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao. Kituo kiko katika: UNIVERSITY CITY RECREATION CENTER _CENTENNIAL COMMONS_ 7210 OLIVE BLVD UNIVERSITY CITY, MO 63130 SAA: MBILI ASUBUHI (8 A.M.)–MOJA JIONI (7 P.M.) SIKU SABA KWA WIKI HADI NOTISI NYINGINE ITOLEWE Vituo vingine vya msaada vimefunguliwa katika: KAUNTI YA ST. LOUIS Kituo cha Hazelwood Civic 8969 Dunn Road Hazelwood, MO 63042                                    SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe JIJI LA ST. LOUIS Chuo cha Ranken Technical _Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee _ 1313 N. Newstead Ave. St. Louis, MO 63113 (Kwenye kona ya Newstead na Page) SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe KAUNTI ST. CHARLES Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB 1025 Country Club Road St. Charles, MO 63303 (I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl) SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe HAKUNA MIADI INAHITAJIKA KUTEMBELEA KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA. WANAOKUJA BILA MIADI WANAKARIBISHWA. Kabla ya kutembelea kituo, tuma ombi na FEMA mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov [https://www.disasterassistance.gov/] au piga simu 800-621-FEMA (3362). Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada.   Kwa mahitaji yanayohusiana moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25—28, FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa: * MSAADA WA KODI YA NYUMBA ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko * MALI YA KIBINAFSI ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko * KURUDISHIWA MALIPO YA MAHALI PA KULALA ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda * MAREKEBISHO YA MSINGI YA NYUMBA KWA WAMILIKI WA NYUMBA ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko * MAHITAJI MENGINE MUHIMU yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo: * OMBI MOJA TU KWA KILA FAMILIA * FEMA HAILIPII CHAKULA KILICHOPOTEA AU KUHARIBIKA Kisheria. Fema hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine            Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA [https://twitter.com/mosema_] na @FEMARegion7 [https://twitter.com/femaregion7]. Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov [https://recovery.mo.gov/] na FEMA.gov/disaster/4665 [https://www.fema.gov/disaster/4665]. _Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi._