FEMA Kituo cha Kupona Maafa cha FEMA huko Davenport Sasa Kimefunguliwa Hadi Oktoba 16

Release Date Release Number
016
Release Date:
Oktoba 7, 2020

DES MOINES, Iowa – Kituo cha Kupona Maafa cha FEMA (DRC) huko Davenport kitakaa wazi kwa siku chache zaidi kuliko ilivyotangazwa hapo awali. Sasa itafungwa kabisa Ijumaa, Oktoba 16 saa 6 asubuhi.

DRC iko katika Kituo cha Majini cha Annie Wittenmyer Family Aquatic Center kilicho katika:

2828 Eastern Ave.

Davenport, IA 52803

Kwenye kona ya Mashariki ya 29th St. na Mashariki Ave ( East 29th St. and Eastern Ave.)

Masaa ya kazi ni Jumatatu mpaka Jumamosi saa 9 asubuhi mpaka saa 6 jioni, Saa za Kati (Central Time) na kufungwa Jumapili.

DRC haitafanya kazi kwa mtindo wa jadi. Kituo hicho kitatoa huduma ya kuendesha gari. Waathirika wanaulizwa kukaa kwenye magari yao wakati wa kutembelea.

Waombaji sio lazima watembelee kituo ili kuwasilisha hati kwa FEMA-wana weza kutuma barua, faksi au kuwasilisha mkondoni kwa DisasterAssistance.gov vile vile. Habari juu ya chaguo hizi zinaweza kupatikana katika barua yao ya FEMA.

Waokoaji ambao tayari wamesajiliwa na FEMA na wame ombwa kutoa nyaraka za ziada wanapaswa kusoma barua yao ya FEMA kwa uangalifu na kuhakikisha wana kila kitu wanacho hitaji wanapofika DRC.

Ikiwa hauelewi barua uliyo pokea kutoka kwa FEMA, piga simu 800-621-3362 (TTY: 800-462-7585) kati ya saa 6 asubuhi na 10 jioni. Saa za Kati (Central Time) na uombe msaada.

Waombaji wote na wafanyikazi wa FEMA watafuata mahitaji ya sasa ya usalama wa hali na wa ndani wa COVID-19. Waombaji lazima wavae vinyago vya uso na watabaki kwenye gari zao wanapokabidhi hati zao kwa wafanyikazi wa FEMA, ambao watavaa vinyago vya uso (au vifuniko vingine vya kufaa uso) na vifaa vya kinga. Wafanyikazi wa FEMA watachukua nyaraka, kuzichambua na kuzirudisha kwa waombaji.

Waombaji wanaweza kujiandikisha kwa njia zifuatazo:

  • Nenda mkondoni kwa DisasterAssistance.gov.
  • Pakua App ya Simu ya FEMA (FEMA Mobile App)   kwa simu mahiri ( smartphones).
  • Piga simu kwa  800-621-3362 (TTY: 800-462-7585) kati ya saa 6 asubuhi na 10 jioni Saa za Kati ( Central Time), siku saba kwa wiki. Waendeshaji kazi wa lugha nyingi wanapatikana.
  • Ikiwa mtu hawezi kujiandikisha mkondoni au kwa simu, usajili katika DRC utapatikana.

Nyaraka pia zinaweza kuwasilishwa kwa njia yoyote ifuatayo

Tuma Barua kwa: Mpango wa Watu Binafsi wa Fema na Kaya, Kituo cha Huduma ya Usindikaji wa Kitaifa, kwa

National Processing Service Center

P.O. Box 10055, Hyattsville MD 20782-7055. 

  • Faks kwa 800-827-8112.
  • Wasilisha kupitia akaunti ya mkondoni ya FEMA. Kuanzisha akaunti mkondoni,  tembelea DisasterAssistance.gov, bonyeza "Angalia Hali" (check status) na ufuate maelekezo.

Utawala wa Biashara Ndogo ya Merika (SBA) inatoa mikopo ya maafa ya riba ya chini kwa wafanya biashara wa saizi zote, mashirika mengi yasiyo ya faida, wamiliki wa nyumba na wapangaji. Uomba kwa https://disasterloanassistance.sba.gov Watu wanaweza pia kupiga 800-659-2955 au barua pepe FOCWAssistance@sba.gov. Watu viziwi au wenye kwana shida ya usikiaji wanao tumia TTY wanaweza kupiga simu 800-877-8339.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho