Mara tu unapotuma ombi la msaada wa FEMA, unapaswa kuwasilisha dai la bima ikiwa bado hujafanya hivyo. FEMA inaweza kuwasiliana nawe ili kuthibitisha habari au kukamilisha ukaguzi wa nyumba, na inaweza kukutuma kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani. FEMA inaposhughulikia ombi lako, utapokea barua ya uamuzi, ambayo unaweza kukata rufaa.
Wasilisha Madai ya Bima
Ikiwa una bima ya wamiliki wa nyumba, wapangaji au ya mafuriko, tuma dai haraka iwezekanavyo. FEMA haiwezi kulipia hasara zinazoshughulikiwa na bima, kwa hivyo wakala anahitaji kuona bima yako inashughulikia nini kabla ya kushughulikia ombi lako. Ikiwa sera yako haishughulikii gharama zako zote, unaweza kustahili msaada wa serikali
Ukaguzi wa Nyumba
Ukiripoti kuwa huwezi au huenda sio salama kuishi nyumbani kwako, FEMA lazima ithibitishe uharibifu kupitia ukaguzi wa nyumba kihalisi au kwa mbali. Wafanyakazi wa FEMA watakupigia simu ili kupanga ukaguzi - kumbuka kuwa wanaweza kupiga simu kutoka kwa nambari isiyojulikana au iliyozuiliwa. Mkaguzi atakuja wakati wewe, mwombaji mwenza wako, au mtu mwingine uliyemteua kwa maandishi yupo
Wakaguzi wa FEMA wamefunzwa kutambua uharibifu unaosababishwa na majanga, lakini hawaamui ikiwa utapata msaada. Ikihitajika, FEMA itaandaa makao yanayofaa, ikijumuisha utafsiri na wakalimani wa ASL, ili kuhakikisha wewe na mkaguzi mnaweza kuwasiliana. Ukaguzi unaweza kuchukua hadi dakika 45 kukamilika.
Kwa habari zaidi kuhusu ukaguzi wa nyumba wa FEMA, tembelea Home Inspections | FEMA.gov, au tazama video inayoweza kupatikana kwa FEMA Accessible: Home Inspections - YouTube.
Usimamizi wa Biashara Ndogo
FEMA inaweza kukutuma kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani (SBA) ili utume ombi la mkopo wa muda mrefu wa majanga wenye riba nafuu. Mara tu FEMA inapokutuma, unapaswa kuwasilisha ombi haraka iwezekanavyo. Mikopo ya SBA ndicho chanzo kikubwa zaidi cha fedha za urejesho za serikali kwa waathirika - na kutuma maombi ya mkopo wa SBA huruhusu FEMA kukuzingatia kwa aina nyingine za msaada.
SBA hutoa mikopo ya majanga ya muda mrefu, yenye riba nafuu kwa biashara za ukubwa wowote, mashirika ya kibinafsi yasiyo ya kibiashara, wamiliki wa nyumba na wapangaji. Haulipishwi kutuma maombi, na si lazima ukubali mkopo ikiwa umeidhinishwa. Ikiwa SBA itakupata hufai, itakurejesha kwa FEMA, ambayo itakutathmini kwa aina za ziada za msaada.
Barua ya Uamuzi
Utapokea barua kutoka kwa FEMA kupitia barua au barua pepe, ikitegemea njia uliyochagua ulipotuma ombi. Barua itaeleza ikiwa FEMA imeona unastahili msaada, kiasi gani, na jinsi msaada huo lazima utumike.
Ikiwa barua yako inasema hustahili, haimaanishi kuwa umekataliwa. Barua hiyo itaeleza jinsi ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo ikiwa hukubaliani nao. Kupata habari zaidi, tembelea Ninawezaje Kukata Rufaa Dhidi ya Uamuzi wa Mwisho? | FEMA.gov.
Msaada Unapatikana
Kupata msaada wa ana kwa ana kwa hatua yoyote ya mchakato huu, tembelea Kituo cha Msaada wa Majanga, ambapo wataalamu kutoka FEMA na SBA wanaweza kujibu maswali, kusaidia kuwasilisha hati na kukuongoza katika mchakato wa kukata rufaa. Vituo vimefunguliwa katika maeneo yaliyoathiriwa kote jimboni - ili kupata moja karibu nawe, tembelea fema.gov/drc.
Ikiwa unahisi mfadhaiko wa kihisia, Nambari ya Msaada wa Majanga ya Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani inapatikana kwa 800-985-5990. Huduma hii isiyolipishwa ya msaada katika lugha nyingi iko wazi 24/7, inaendeshwa na Usimamizi wa Matumizi Mabaya ya Dawa na Huduma za Afya ya Akili. Watumiaji wa Lugha ya Ishara ya Marekani wanaweza kupiga simu kwa nambari ya msaada kutumia simu ya video kwa 800-985-5990, au kwa kuchagua chaguo la "ASL Now" kwenye tovuti kwa www.samhsa.gov/find-help/disaster-distress-helpline.
JInSI YA KUTUMA MAOMBI
Ikiwa unaishi katika kaunti ya Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham au Windsor na uliathiriwa na dhoruba kali mwezi wa Julai huko Vermont, FEMA inaweza kukusaidia na gharama za makao ya muda, marekebisho ya msingi ya nyumba na mahitaji mengine yanayohusiana na majanga. Ili kutuma ombi, tembelea DisasterAssistance.gov, pakua FEMA App kutoka Apple App Store au Google Play Store, au piga simu kwa laini ya msaada ya FEMA bila malipo kwa 800-621-3362 na tafsiri ya lugha inapatikana. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.
Ikiwa anwani yako haiko katika eneo lililoteuliwa kwa sasa, bado unaweza kutuma ombi kwa kupiga Simu kwa laini ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362. Hii itakuruhusu kuendelea ikiwa kaunti yako itaongezwa kwenye tangazo.
Kupata msaada ana kwa ana, tembelea Kituo cha Msaada wa Majanga, ambapo wataalamu wa FEMA wanaweza kusaidia katika kutuma maombi, kujibu maswali na kutoa marejeleo ya rasilimali. Ili kupata kituo karibu nawe, tembelea fema.gov/drc.
FEMA itaomba:
- Nambari ya simu ya sasa unayoweza kupatikana;
- Anwani ya ulipokuwa ukiishi wakati wa janga;
- Anwani ya unapoishi sasa;
- Nambari yako ya Ruzuku ya Serikali;
- Orodha ya uharibifu na hasara;
- Taarifa za benki (ukichagua kuweka pesa moja kwa moja); na
- Ikiwa una bima, nambari yako ya sera, wakala na/au kampuni ya bima.
Timu za Kusaidia Walionusurika Majanga ya FEMA zinatembelea nyumba katika jamii zote jimboni ili kuwasaidia wakazi kutuma maombi ya usaidizi. Ili kujifunza jinsi wanavyoweza kusaidia - na jinsi ya kuwatofautisha kutoka kwa walaghai - tembelea FEMA Disaster Survivor Assistance Crews Support Vermont Communities | FEMA.gov.
Kupata video kuhusu jinsi ya kutuma ombi, nenda kwenye FEMA Accessible: Three Ways to Register for FEMA Disaster Assistance - YouTube.
Kwa habari mpya zaidi kuhusu urejesho wa Vermont, tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Region 1 katika Twitter twitter.com/FEMARegion1 au ukurasa wa Facebook wa FEMA katika facebook.com/FEMA.
Fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont kwenye Twitter katika twitter.com/vemvt na kwenye Facebook katika facebook.com/VermontEmergencyManagement.
FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaozungumza lugha nyingi wanapatikana.