Kituo cha Springfield kinapatika katika:
Springfield Health Center
100 River Street
Springfield, VT 05156
Vituo Vingine vya Msaada Vitabakia wazi saa mbili asubuhi (8 a.m) hadi saa moja jioni (7 p.m.) kila siku
Waterbury Armory
294 Armory Drive
Waterbury, VT 05676
ASA Bloomer Building
88 Merchants Row, Suite 330
Rutland, VT 05701
Barre Auditorium
16 Auditorium Hill
Barre, VT 05641
Barton Memorial Building
17 Village Square
Barton, VT 05822
Jamaica Fire Department
4017 VT-30
Jamaica, VT 05343
FEMA huhamisha Vituo vya Msaada wa Majanga kulingana na mahali vinapohitajika zaidi. FEMA hufanya kazi kwa karibu na washirika wa jimbo na manispaa katika kubainisha maeneo hayo. Mara tu eneo linapoanza kuwa na kiasi kidogo cha ziara za usajili, FEMA na jimbo huratibu maeneo mapya ambapo kituo kinaweza kupokea ziara zaidi kutoka kwa wale wanaohitaji usaidizi.
Vituo vyote vinaweza kufikiwa na watu wenye ulemavu na mahitaji ya kutenda, na vina vifaa vya teknolojia ya usaidizi. Ikiwa unahitaji makao ya kuridhisha au mkalimani wa lugha ya ishara, tafadhali piga simu kwa 833-285-7448 (bonyeza 2 kwa Kihispania).
Wawakilishi kutoka Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani (SBA) pia watakuwa kituoni kueleza jinsi ya kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu ya SBA kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara na mashirika yasiyo ya kibiashara ya kibinafsi, na kutoa maelezo kuhusu kujenga upya ili kufanya nyumba zistahimili majanga zaidi.
Huhitaji kutembelea DRC ili kutuma maombi ya msaada wa FEMA. Kutuma ombi bila kutembelea kituo, piga simu kwa nambari ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362, nenda mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au upakue FEMA App. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi. Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya msaada wa serikali ni Septemba 12, 2023.
FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wa lugha mbali mbali wanapatikana.