Makataa ya Kujiandikisha kwa ajili ya Usaidizi wa FEMA Imeongezwa hadi Novemba 7

Release Date Release Number
16
Release Date:
Oktoba 3, 2022

Wapangaji na wamiliki wa nyumba katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles ambao waliathiriwa na mafuriko Julai 25-28 sasa wana hadi Jumatatu, Novemba 7, 2022, kutuma maombi ya Msaada wa Majanga ya FEMA. Kufikia Oktoba 3, 2022, FEMA imeidhinisha zaidi ya $36.4 milioni katika ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi kwa zaidi ya familia 11,900 katika eneo la St. Louis.

Tuma maombi mtandaoni kupitia DisasterAssistance.gov, kwa kupiga simu kwa 800-621-3362 au kwa kutumia FEMA mobile app.

Ikiwa unatumia huduma ya kupitisha ujumbe, kama vile kupitisha ujumbe kupitia video (VRS), simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo.

Kwa mahitaji ambayo hayashughulikiwa na bima au vyanzo vingine, FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa ajili ya:

  • Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
  • Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
  • Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
  • Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
  • Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni

Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo:

  • Ombi moja tu kwa kila familia
  • FEMA hailipii chakula kilichopotea au kuharibika
  • Kisheria, FEMA hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine

Unapotuma ombi kwa FEMA, uwe na maelezo yafuatayo tayari:

• Nambari ya simu ambayo unaweza kupigiwa

• Anwani wakati wa mafuriko

• Anwani unapoishi sasa

• Nambari ya Ruzuku ya Serikali ya Mtu mmoja katika familia

• Orodha ya msingi ya uharibifu na hasara

• Taarifa za benki ukichagua kuwekewa moja kwa moja pesa za FEMA kwenye benki

• Taarifa za Bima ikiwa una bima, ikijumuisha nambari ya sera

Ikiwa una bima ya wamiliki nyumba, mpangaji au mafuriko, unapaswa kuwasilisha dai haraka iwezekanavyo. FEMA haiwezi kulipia tena hasara zinazolipiwa na bima. Ikiwa sera yako haishughulikii gharama zako zote za uharibifu, unaweza kustahili usaidizi wa serikali.

Kumbuka kuweka risiti kutoka kwa ununuzi wote unaohusiana na kusafisha na kurekebisha.

Kwa video inayoweza kupatikana ya jinsi ya kutuma ombi la usaidizi, tembelea youtube.com/watch?v=WZGpWI2RCNw.

Kwa masasisho ya majanga kutoka FEMA, fuata @FEMAregion7 kwenye Twitter, na uwashe arifa za simu. Tembelea tovuti ya majanga kwa fema.gov/disaster/4665.

Kwa masasisho ya majanga kutoka kwa Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Jimbo la Missouri (SEMA), fuata @MOSEMA_kwenye Twitter, na uwashe arifa za simu. Recovery.MO.gov inaendelea kuwa mahali pa kwenda kwa watu wa Missouri ili kupata taarifa na rasilimali zinazohusiana na maafa kwa urahisi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho