CHAGUO ZA KUTHIBITISHA UTAMBULISHO WAKO KWA FEMA [https://www.fema.gov/sw/fact-sheet/options-verify-your-identity-fema] Release Date: Aug 4, 2023 Unapotuma ombi la msaada wa majanga, lazima FEMA ithibitishe utambulisho wako ili kuhakikisha kuwa unapokea msaada unaostahili. Ikiwa FEMA haiwezi kuthibitisha utambulisho wako kupitia rekodi za umma, unaweza kuhitajika kuwasilisha hati za ziada. HATI ZINAZOKUBALIKA ZA KUTHIBITISHA UTAMBULISHO Ili kuthibitisha utambulisho wako, tumia FEMA nakala za: * Hati kutoka kwa Usimamizi wa Ruzuku ya Serikali au taasisi nyingine ya serikali inayoonyesha tarakimu zako kamili au nne za mwisho za Nambari yako ya Ruzuku ya Serikali; * Kitambulisho cha Serikali au kilichotolewa na jimbo NA Kadi yako ya Ruzuku ya Serikali; * Orodha ya malipo ya mwajiri iliyo na tarakimu kamili au nne za mwisho za SSN yako; * Utambulisho wa kijeshi; * Leseni ya ndoa (kuthibitisha jina lako kabla ya ndoa); au * Pasipoti ya Marekani. Ikiwa unatuma maombi kwa niaba ya mtoto raia wa Marekani aliye chini ya miaka 18, tumia FEMA yafuatayo: * Hati zozote zilizoorodheshwa hapo juu ikiwa katika jina la mtoto; au * Cheti cha kuzaliwa cha mtoto NA nakala ya kadi yake ya Ruzuku ya Serikali, au hati kutoka kwa Usimamizi wa Ruzuku ya Serikali au taasisi nyingine ya serikali ambayo ina tarakimu kamili au nne za mwisho za SSN ya mtoto. JINSI YA KUWASILISHA HATI ZAKO Hati zote zinaweza kutumwa kwa FEMA kwa mojawapo ya njia hizi: * PAKIA kwenye akaunti yako ya DisasterAssistance.gov [https://www.disasterassistance.gov/]; * BARUA kwa: FEMA National Processing Service Center, P.O. Box 10055, Hyattsville, MD 20782-7055; * FAKSI kwa 800-827-8112; au, * WASILISHA ANA KWA ANA KWENYE KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA. Ili kupata kituo karibu nawe, tembelea fema.gov/drc [http://www.fema.gov/drc]. FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaozungumza lugha nyingi wanapatikana.