KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA CHA FEMA KINAFUNGULIWA KATIKA KAUNTI YA WINDSOR [https://www.fema.gov/sw/press-release/20230804/fema-disaster-recovery-center-opens-windsor-county] Release Date: Agosti 4, 2023 Kituo cha Msaada wa Majanga kitafunguliwa springfield Agosti 4 kusaidia wakaazi wa Vermont walioathiriwa na mafuriko kuanza kurudia hali ya kawaida. DRC ya pamoja, kituo cha muda kilichoanzishwa kwa ushirikiano kati ya Springfield, jimbo la Vermont na FEMA, itasaidia waathiriwa kutuma maombi ya msaada wa FEMA, kupakia hati na kujibu maswali ana kwa ana. KITUO CHA SPRINGFIELD KINAPATIKANA KATIKA: Springfield Health Center 100 River Street Springfield, VT 05156 VITUO TAYARI VIMEFUNGULIWA KATIKA: Waterbury Armory 294 Armory Drive Waterbury, VT 05676 ASA Bloomer Building 88 Merchants Row, Suite 330 Rutland, VT 05701 Barre Auditorium 16 Auditorium Hill Barre, VT 05641 Flood Brook School 91 VT-11 Londonderry, VT 05148 Twinfield Union School 106 Nasmith Brook Road Plainfield, VT 05667 Barton Memorial Building 17 Village Square  Barton, VT 05822 VITUO VYOTE VINAFUNGULIWA SIKU 7 KWA WIKI, SAA MBILI ASUBUHI  (8 A.M) HADI SAA MOJA JIONI (7 P.M.) Vituo vyote vinaweza kufikiwa na watu wenye ulemavu na mahitaji ya kutenda, na vina vifaa vya teknolojia ya usaidizi. Ikiwa unahitaji makao ya kuridhisha au mkalimani wa lugha ya ishara, tafadhali piga simu kwa 1-833-285-7448 (bonyeza 2 kwa Kihispania). Wawakilishi kutoka Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani (SBA) pia watakuwa kituoni kueleza jinsi ya kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu ya SBA kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara na mashirika yasiyo ya kibiashara ya kibinafsi, na kutoa maelezo kuhusu kujenga upya ili kufanya nyumba zistahimili majanga zaidi. Huhitaji kutembelea DRC ili kutuma maombi ya msaada wa FEMA. Kutuma ombi bila kutembelea kituo, piga simu kwa nambari ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362, nenda mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov] au upakue FEMA App [https://www.fema.gov/about/news-multimedia/mobile-products]. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.  FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wa lugha mbali mbali wanapatikana.