KITUO KIPYA CHA MSAADA WA MAJANGA CHAFUNGULIWA KATIKA JIJI LA ST. LOUIS: MASAA KATIKA VITUO VYOTE VYA MSAADA WA MAJANGA YATABADILIKA JUMATATU [https://www.fema.gov/sw/press-release/20220909/new-disaster-recovery-center-opens-st-louis-city-hours-all-disaster-recovery] Release Date: Septemba 9, 2022 Kituo kipya cha Msaada wa Majanga cha FEMA kitafunguliwa JUMAMOSI, SEPTEMBA 10, katika Jiji la St. Louis ili kutoa usaidizi wa ana kwa ana kwa watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25—28 na dhoruba kali. Wataalamu wa Misaada kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani watatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao. Vituo vya msaada wa majanga vinapatikana katika: KITUO CHA SALVATION ARMY TEMPLE 2740 ARSENAL ST ST. LOUIS, MO 63118 (KARIBU NA KONA YA ARSENAL NA CALIFORNIA) MASAA YA JUMAMOSI: SAA MBILI ASUBUHI (8 A.M.) – SAA KUMI NA MOJA JIONI (5 P.M.) Kuanzia JUMATATU, SEPTEMBA 12, masaa mapya za vituo vyote vya msaada itakuwa: JUMATATU – IJUMAA, SAA MBILI ASUBUHI (8 A.M.) – SAA KUMI NA MBILI JIONI (6 P.M). JUMAMOSI, SAA MBILI ASUBUHI (8 A.M.) – SAA KUMI NA MOJA JIONI (5 P.M.) INAFUNGWA JUMAPILI Vituo vingine vya msaada vimefunguliwa katika maeneo haya: JIJI LA ST. LOUIS Chuo cha Ranken Technical _Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee _ 1313 N. Newstead Ave. St. Louis, MO 63113 (Kwenye kona ya Newstead na Page) KAUNTI YA ST. LOUIS Kituo cha Urban League Empowerment 9420 W. Florissant Ave. Ferguson, MO 63136 Kituo cha University City Recreation _Centennial Commons_ 7210 Olive Blvd. University City, MO 63130 Kituo Hazelwood Civic 8969 Dunn Road Hazelwood, MO 63042 KAUNTI YA ST. CHARLES Kituo cha Manispaa ya O’Fallon 100 N. Main St. O’Fallon, MO 63366 (Kiingilio cha Kusini-mashariki) Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB 1025 Country Club Road St. Charles, MO 63303 (I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl) ENEO LA DDRB LITAFUNGWA KABISA JUMATANO, SEPTEMBA 14, SAA KUMI NA MBILI JIONI (6PM). HAKUNA MIADI INAHITAJIKA KUTEMBELEA KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA. WANAOKUJA BILA MIADI WANAKARIBISHWA Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada. Ikiwa unahitaji msaada kutuma maombi, FEMA inaweza kukusaidia katika Kituo cha Msaada wa Majanga. Tuma ombi na FEMA mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov [https://www.disasterassistance.gov/] au piga simu 800-621-FEMA (3362). FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa: * MSAADA WA KODI YA NYUMBA ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko * MALI YA KIBINAFSI ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko * KURUDISHIWA MALIPO YA MAHALI PA KULALA ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda * MAREKEBISHO YA MSINGI YA NYUMBA KWA WAMILIKI WA NYUMBA ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko * MAHITAJI MENGINE MUHIMU yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo: * OMBI MOJA TU KWA KILA FAMILIA * FEMA HAILIPII CHAKULA KILICHOPOTEA AU KUHARIBIKA * KISHERIA, FEMA HAIRUHUSIWI KULIPIA TENA MALIPO YA BIMA AU USAIDIZI ULIOTOLEWA NA VYANZO VINGINE WAMILIKI WA NYUMBA NA WAPANGAJI: Baada ya kutuma maombi na FEMA Ikiwa umetumwa kwa SBA kwa ajili ya mkopo wa majanga, tafadhali wasilisha ombi. Kuwasilisha ombi la SBA hukuwezesha kuzingatiwa kwa ajili ya ruzuku za ziada ikiwa utanyimwa mkopo wa SBA. Ikiwa unastahili kupata mkopo, utakuwa na rasilimali hiyo ikiwa utachagua kuikubali. Usaidizi wa ombi lako la SBA unapatikana katika Vituo vyovyote vya Msaada wa Majanga.                               Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA [https://twitter.com/mosema_] na @FEMARegion7 [https://twitter.com/femaregion7]. Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov [https://recovery.mo.gov/] na FEMA.gov/disaster/4665 [https://www.fema.gov/disaster/4665]. _Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi._