FEMA INAFUNGUA KITUO CHA KUPONA MAAFA KATIKA KAUNTI YA TAMA [https://www.fema.gov/sw/press-release/20201001/fema-inafungua-kituo-cha-kupona-maafa-katika-kaunti-ya-tama] Release Date: Septemba 30, 2020 DES MOINES, IOWA – Kituo cha Kupona Maafa (DRC) kitafunguliwa saa 9 alasiri huko Meskwaki Casino RV Park Jumatatu, Oktoba 5, kuwapa waokokaji kutoka chaguzi kali za dhoruba za Agosti 10 kuwasilisha nyaraka za maombi yao ya msaada wa majanga. DRC itakuwa wazi kwa muda mdogo na ina wafanyikazi wa FEMA ambao wanaweza kuchanganua nyaraka na kujibu haraka maswali juu ya mipango ya msaada wa maafa. Itafungwa kabisa Jumamosi, Oktoba 10 saa 6 asubuhi. DRC haitafanya kazi kwa mtindo wa jadi. Kituo hicho kitatoa huduma ya kuendesha gari. Waathirika wana ulizwa kukaa kwenye magari yao wakati wa kutembelea. Waombaji sio lazima watembelee kituo ili kuwasilisha hati kwa FEMA-wanaweza kutuma barua, faksi au kuwasilisha mkondoni kwa DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov/] vile vile. Habari juu ya chaguo hizi zinaweza kupatikana katika barua yao ya FEMA. Waokoaji ambao tayari wame sajiliwa na FEMA na wame ombwa kutoa nyaraka za ziada wanapaswa kusoma barua yao ya FEMA kwa uangalifu na kuhakikisha wana kila kitu wanacho hitaji wanapo fika DRC. Ikiwa hauelewi barua uliyopokea kutoka kwa FEMA, piga simu 800-621-3362 (TTY: 800-462-7585) kati ya saa 6 asubuhi na 10 jioni. Saa za Kati, na uombe msaada. FEMA DRC iko: MESKWAKI CASINO RV PARK 1504 305TH ST TAMA, IA 52339 (HIFADHI YA RV IKO NYUMA YA STAHA YA MAEGESHO YA KASINOASINO NA UWANJA WA MAEGESHO WA KASINO ) Saa za DRC ni Jumatatu hadi Jumamosi, 9 asubuhi hadi 6 jioni. Saa za Kati (Central Time ) Ilifungwa Jumapili Waombaji wote na wafanyikazi wa FEMA watafuata mahitaji ya sasa ya usalama wa hali na wa ndani wa COVID-19. Waombaji lazima wavae vinyago vya uso na watabaki kwenye gari zao wanapokabidhi hati zao kwa wafanyikazi wa FEMA, ambao watavaa vinyago vya uso (au vifuniko vingine vya kufaa uso) na vifaa vya kinga. Wafanyikazi wa FEMA watachukua nyaraka, kuzichambua na kuzirudisha kwa waombaji. Waombaji wanaweza kujiandikisha kwa njia zifuatazo: * Nenda mkondoni DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov/]. *  Pakua App ya Simu ya FEMA kwa simu mahiri (smartphone) * Piga simu kwa 800-621-3362 (TTY: 800-462-7585) kati ya saa 6 asubuhi na 10 jioni Saa za Kati, siku saba kwa wiki. Waendeshaji wa lugha nyingi wana patikana. Ikiwa mtu hawezi kuji andikisha mkondoni au kwa simu, usajili katika DRC utapatikana. Nyaraka pia zinaweza kuwasilishwa kwa njia yoyote ifuatayo: * Tuma  Barua kwa: Mpango wa watu binafsi na kaya wa FEMA,( Kituo cha Huduma ya Usindikaji wa Kitaifa),(National Processing Service Center, P.O. Box 10055, Hyattsville MD 20782-7055.  * Au faks kwa 800-827-8112. * Au uwasilishe kupitia akaunti ya mkondoni ya FEMA. Kuanzisha akaunti mkondoni, tembelea DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov/], bonyeza "Angalia Hali" (check status) na ufuate maelekezo